37. JINSI YA KUONDOA MBA KWA KUTUMIA MUARUBAINI (NEEM LEAVES)

adsense 336x280 Tumekua tukiongelea sana suala la kuondoa mba lakini bado kuna wengine wanapata changamoto ya kushindwa kuondoa mba kwenye nywele zao. Mba unatesa sana, unakua huna raha, kila muda unajikuna na wengine huishia kunyoa nywele zao kisa mba. Leo tuangalie njia nyingine ambayo unaweza kufanya kuondoa mba kabisa ambayo pia ni tiba nzuri kwa nywele, mapunye, mba, vidonda kichwani nk.

MAHITAJI
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Majani ya muarubaini
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Mafuta ya nazi/Mafuta ya mnyonyo
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Shower cap

JINSI YA KUFANYA
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Chukua majani yako ya mwarobaini yaoshe vizuri
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Chemsha majani hayo ndani ya dk 10 hadi 15
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Chuja mchemsho huo kisha upate maji ya miarobaini
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️ Ongeza vijiko viwili vya mafuta (utakayochagua wewe)
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Weka mchanganyiko huo ukae masaa 12 ukiwa umetulia ili kupunguza nguvu
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Baadae osha kichwani huku ikisugua ngozi ya kichwa  na mchanganyiko huo
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Ukimaliza vaa shower cap na kaa nayo kwa muda wa dk 30
๐Ÿงš๐Ÿป‍♂️Kisha osha nywele zako na maji safi

NB: Majani ya muarobaini yana faida nyingi sana kwenye nywele ikiwa ni pamoja na;
๐ŸƒKutoa na kuzuia mba
๐ŸƒHuzuia nywele kukatika
๐ŸƒKutibu mapunye, vidonda na miwasho
๐ŸƒKufanya ngozi ya kichwa ilainike na kurelax. adsense 336x280

0 Response to "37. JINSI YA KUONDOA MBA KWA KUTUMIA MUARUBAINI (NEEM LEAVES) "

Post a Comment