89. KWA NINI UKATE NCHA ZA NYWELE

adsense 336x280

Katika kushauriwa ukuzaji wa nywele nzuri na zenye afya mara nyingi tunakuta tunaambiwa tukate ncha za nywele, lakini kukata ncha hizi za nywele kunasaidia vipi kukuza nywele? na je ni mara ngapi unatakiwa kukata hizi ncha?
TUJIFUNZE KIDOGO.....
Ncha za nywele ni zile nywele zilizopo mwishoni kabisa hizi huwa nyepesi kuliko nywele zote ni kama zimesha kufa, wengi hujiuliza kwanini nywele hizi ni nyepesi?
๐Ÿ‘‰๐Ÿป Ni kutokana  na matumizi ya moto na kuchana nywele vibaya, hivyo ili kukuza nywele zako kuwa ndefu na zenye afya ni vyema ukakata ncha. Ni kama katika kukata miti au michongoma ile ya juu hukua nakuwa mibaya wakati huku chini inashamiri kwa kupata matunzo mazuri lakini kama utaiacha ile ya juu basi itaharibu show nzima ya hii ya chini.
๐Ÿ‘‰๐ŸปNcha za nywele mara nyingi huwa zimechoka na hata rangi yake kubadilika, mara nyingi ncha huwa lighter kuliko nywele za chini, zina haribu muonekano mzuri wa nywele
๐Ÿ‘‰๐Ÿป Hata ukitumia pesa kiasi gani katika salon kama ncha za nywele zako hujakata zitaonekana lifeless hazitopendeza hata kidogo lakini pia husababisha ukatikaji wa nywele.
๐Ÿ‘‰๐ŸปPia huwezi kutibu Ncha kwa kufanya hair treatments, unachotakiwa kufanya ni kuzikata tu, utapoteza muda na fedha zako bure, split ends hazina tiba

JINSI YA KUEPUKA NCHA ZA NYWELE AU NYWELE KIUJUMLA
๐Ÿ‘‰๐ŸปKata ncha
๐Ÿ‘‰๐ŸปPaka mafuta nywele zako kabla ya kuziosha
๐Ÿ‘‰๐ŸปChana  nywele zako taratibu
๐Ÿ‘‰๐ŸปTumia chanuo lenye meno makubwa kuchana nywele
๐Ÿ‘‰๐ŸปPunguza matumizi ya moto katika nywele
๐Ÿ‘‰๐ŸปKula chakula bora na kunywa maji ya kutosha
adsense 336x280

0 Response to "89. KWA NINI UKATE NCHA ZA NYWELE"

Post a Comment